Mfanyabiashara
Henry Munisi mkazi wa jiji la Mbeya mwenye umri wa miaka 30
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa
shtaka la kuchapisha taarifa za uongo zinazomhusisha Rais Dkt, John
Magufuli na upotevu wa Sh 1.5 Trilioni.
Munisi
anashtakiwa kwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook taarifa za
uongo zinazomhusu Rais Magufuli akizihusisha na ununuzi wa ndege za
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).
Wakili
wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita akitoa madai yake mbele ya Hakimu
mkazi mwandamizi, Salum Ally amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo
Desemba 28, 2018 akiwa Jijini Mbeya.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kuchapisha katika ukurasa wake wa Facebook taarifa
inayosomeka “Jinsi Magufuli alivyochota Tril, 1.5 za ATCL akitumia
ujanja wake wa kuleta ndege ili atuibie.”
Wakili
Mwita ameiambia Mahakama kuwa mshtakiwa alifanya hivyo huku akijua
taarifa hizo ni za uongo na zina lengo la kupotosha umma.
Baada
ya kusomewa mashtaka alikana kuhusika na tukio hilo, ambapo wakili wa
serikali, Mwita alidai kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe
nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo.
Hakimu
Ally aliagiza mshatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za
utambulisho watakaosaini bondi ya sh. 500,000, ambapo alifanikiwa
kutimiza na kuachiwa kwa dhamana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 6, mwaka huu.
Mpekuzi.
Comments