Walimu wa tehama watakiwa kuelimisha vijana juu ya matumizi yalio sahihi.

Image may contain: 1 person
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dr Idrissa Muslim Hija amewataka walimu wa teknolojia ya tehama kuwaelimisha vyema vijana wao juu ya matumizi sahihi ya teknolojia hiyo ili kwenda sambamba na makusudio ya kuanzishwa kwa teknolojia hiyo.

Amesema kumekuwepo tatizo kwa baadhi ya walimu na wanafunzi kuwa na tabia ya kutumia vibaya teknolojia hiyo kwa kuweka au kuangalia vitu visivyostahiki, hali inayopelekea kuporomoka maadili ya kizanzibari.

Akizungumza katika maadhimisho ya pili ya walimu wa Tehama katika ukumbi wa skuli ya sekondari Kwarara Dr Idrissa amesema Wizara inatoa onyo Kali kwa wanaotumia vibaya teknolojia hiyo na kuwataka kuwacha mara moja.


Aidha amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kujenga miundombinu ya Elimu na tehama ili kuondosha matatizo mbalimbali ya kielimu na kuhakikisha inatoa Elimu bora nchini.

Amesema skuli mbalimbali zinazojengwa hivi sasa zimekuwa zikiwekewa miundombinu ya tehama ili kurahisisha matumizi ya tehama wakati utakapofika katika skuli hizo.

Hata hivyo amewashukuru wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Serikali ya Korea kwa kutia Elimu ya matumizi ya tehama katika Elimu .

Nao walimu wa tehama katika Risala yao wamesema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana bado kuna matatizo ikiwemo kukosekana mazingira rafiki ya skuli pamoja na vifaaa vya maabara na kukosekana kwa mtandao kwa ajili ya kujisomea.

Nae Mkuu wa Kituo cha Habari katika Elimu bi Sabrina Masoud Suleiman amesema lwngo la kuanzishwa kituo hicho ni kuandaa mitaala mbalimbali kwa kufuata utaratibu wa Wizara kwa lengo la kuielimisha jamii.
Image may contain: 6 people, people smilingImage may contain: 6 people

Comments