Kamati BLW yazitaka taasisi za sheria kusaidia wananchi.

KAMATI ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalumu ya Baraza la Wawakilishi, imezitaka taasisi zinazosimamia masuala ya sheria na utawala bora, kupanua wigo wa kitaalamu ili kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Machano Othman Said, alisema kamati hiyo imebaini kuna baadhi ya mambo ya kiutendaji katika eneo hilo yanahitaji kuongezewa nguvu  ili wananchi wapate huduma bora.
Alisema mfumo huo utasaidia kuleta tija na kuimarisha utawala bora na demokrasia nchini.
Alisema watakutana na baadhi ya watendaji na viongozi wa taasisi za sheria ili kujadiliana ili kuimarisha zaidi eneo hilo.
Mbali na hayo, alisema kamati hiyo pia imebaini kuna baadhi ya masuala ya sheria,  yanafanyiwa kazi vizuri kiutendaji.
Alisema kwa sasa kamati hiyo ipo Tanzania Bara kujifunza mambo mbali mbali ya maendeleo katika taasisi za mahakama, utumishi wa umma na TAKUKURU.
Zanzibarleo.

Comments