Msemaji
wa Jeshi la polisi, DCP Ahmed Msangi, amesema suala la makamanda
watatu wa polisi ambao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,
alitangaza kuwavua nyadhifa zao lipo mezani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP), Simon Sirro, likisubiri utatuzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Msangi alisema kwa nafasi
yake hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa tayari liko mezani kwa IGP
ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kulizungumzia na kulisimamia.
“Mimi
nikiwa msemaji wa polisi siwezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko
mezani kwa IGP,” alisema alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa agizo la
Lugola.
Wiki
iliyopita, Lugola alitangaza kutengua uteuzi wa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Polisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,
Emmanuel Lukula na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi.
Licha ya agizo hilo la Lugola, makamanda hao waliendela kubaki ofisini.
Licha ya agizo hilo la Lugola, makamanda hao waliendela kubaki ofisini.
Siku
chache baadaye Lugola alipoulizwa juu ya agizo lake kutotekelezwa,
alisema: “Sina taarifa kwamba agizo langu halijatekelezwa, lakini
nilimpa IGP muda wa utekelezaji, kwa hiyo naamini litatekelezwa. Saa
nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka, na mimi ninayo.
Utekelezaji unaendelea.”
Comments