Akifariji familia ya marehemu i, Castico alisema vitendo hivyo ni vya
kinyama na kikatili na jamii inapaswa kuungana kupambana navyo.
Alisema vijana wanapaswa kujielewa namna ya kutumia nguvu zao katika
kazi za halali na sio kuwabaka, kulawiti na kuwaua wanawake na watoto
wasio na hatia.
Alisema vitendo hivyo vinaiweka Zanzibar katika sura mbaya katika macho ya jamii ya kimataifa.
“Sijui tunakwenda wapi na jamii hii itakuaje iwapo mambo haya
yataendelea, kila siku wanajaribu kubuni mbinu tofauti za udhalilishaji
na sasa yamekuwa ni mauaji ambayo wanafanyiwa wanawake wazee na watoto
wasio na makosa yoyote,” alisema.
Alisema wanawake ndio wazazi, walezi na watunzaji wa familia lakini
wanahujumiwa kwa kila aina, hivyo mshikamano wa malezi ni muhimu ili
kupata vijana bora wa baadae.
“Kwa nini haya mambo yanajirejea, lazima masheha, wazee wa mitaa na
waratibu muangalie kwa namna gani mtaweka ulinzi shirikishi na yeyote
atakayeoneka anatembea usiku mkubwa mumuhoji na ikiwezekana achukuliwe
hatua,” alisema.
Alisema amani na utulivu ndio msingi wa maendeleo hivyo wananchi waungane kuhakikisha hali hiyo inaendelea.
Baadae Castico akiambatana na Naibu wake, Shadia Mohammed, Naibu
Katibu Mkuu, Mwajuma Majid na Mkurugenzi Wanawake na Watoto, Nasima Haji
Chum, walifika kijiji cha Mangapwani kumuangalia mtoto wa kike ambaye
ni kiziwi aliyebakwa hivi karibuni.
znazibarleo.
Comments