Askofu
Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe
amesema kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikiishi kama nchi ya laana
kutokana na matunda yake pamoja na tabu zake kuliwa na nchi
isiyojulikana.
Askofu
Kakobe ameyasema hayo leo Jumanne Januari 22, 2019 katika mkutano wa
wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini nchini
unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Askofu
Kakobe amesema kwa miaka mingi matunda ya nchi ikiwamo madini yamekuwa
yakiliwa na mataifa ya nchi nyingine na kuacha mashimo yasiyo na faida
kwa nchi.
“Lakini
ni jambo la kushukuru kwa sababu Mungu amemuinua shujaa Rais John
Magufuli ambaye amekataa kwamba tuachiwe mashimo na urithi wetu wachukue
mataifa mengine na suala hili linahitaji ushujaa sana,” amesema.
Amesema
ukiingia katika habari za matunda ya nchi kubaki ndani ya taifa husika
umetangaza vita ambayo miongoni mwake ni ile ya kiuchumi.
Pia,
Askofu Kakobe alizungumzia tabia ya baadhi ya watu wanaopenda kuona
Rais Magufuli anapingwa katika kila jambo licha ya kuwa kuna mazuri
mengi anayoyafanya, kama waungwana hawatakiwi kupinga kila jambo hata
kama wana hoja bali wanapaswa kutafuta mazuri ya kupongeza ili walete
hoja.
“Hata
Biblia inasema tutangulize yaliyo mema hata kama una hasira naye, hata
Yesu Kristo alipokuwa anatoa ujumbe kwa makanisa saba alikuwa anaanza
kupongeza mazuri hata kabla ya kuinua jambo lolote la kupinga,
atakayekuwa anapinga atakuwa ni mkorofi na hata ukiwa na hoja itakuwa
ngumu kusikilizwa,” amesema Askofu Kakobe.
Amesema
Mungu ameipendelea Tanzania katika upande wa ugawaji mipaka na kuifanya
kuwa nchi yenye kuvutia kwa kuipatia urithi wa aina mbalimbali.
“Hata ukiangalia kule Moshi namna ramani ilivyopindapinda ili kuruhusu Mlima Kilimanjaro uwe wa kwetu,” amesema.
Amesema
kwa miaka mingi watu wamekuwa wakiita Tanzania nchi maskini lakini Rais
Magufuli amethibitisha kuwa Tanzania ni nchi tajiri yenye uwezo wa
kutoa misaada kwa nchi nyingine.
“Mimi
nafikiri unapoanza kupambana na suala hili, uanze kufanyia kazi kwanza
fikira za mtu. Kadiri tunapozidi kutamka vitu vizuri ndiyo tunazidi
kuvichochea,” amsema.
Mpekuzi.
Comments