Aliyasema hayo katika Ukumbi wa Elimu mbadala Rahaleo wakati akizungumza na watendaji wa baraza la mitihani Zanzibar.
Alieleza kuwa tukio lililotokea la kuvuja kwa mitihani limeisababishia
serikali hasara kubwa , ambapo zaidi ya milioni 250 zimetumika katika
kuanza kutunga mitihani hadi kufikia hatua ya kufanyika.
Alisema mbali na kuingia hasara serikali bali mpaka wanafunzi na walezi nao wamethirika kwa namna moja au nyengine, hivyo aliwataka watendaji hao kutoa ushirikiano kuhakikisha wanasaidia kupatika na hujuma hizo.
“Mtihani ni roho ya nchi endapo tutavujisha tutakuwa na taifa legelege ambalo litashindwa kuzalisha wataalamu hapo baadae katika kukuza uchumi wa nchi”.
Alifahamisha kuwa taarifa za uvujaji wa mitihani hiyo zilitoka kwa raia mwema , na kueleza kuwa baadhi yao waliuza mitihani kwa bei ya 20,000.
Sambamba na hilo pia alisema hivi sasa suala hilo wameachiwa kikosi cha ulinzi na usalama ili kujua nani anahusika na kadhia hiyo .
Kwa upande wa Naibu Wazir wa Elimu Mhe. Mmanga Mjengo Mjrawiri ameseme kitendo kilichofanyika ni upungufu wa maadili , hivyo wizara haitokuwa tayari kuona inatiwa dosari na watu wachache wasiotaka maendeleo ya elimu.
Nae Mkurugenzi wa Baraza la mitihani Bw. Zueir Juma Khamis alisema kuwa suala la mitihani linahatua nyingi ambazo zinapitia, Hivyo popote palipohusika na tuhuma hizo patashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Comments