Waziri Luhaga Mpina Aibua Kashifa ya Kuingizwa Nyama Mbovu Nchini.....Asema Kamwe Tanzania Haiwezi Kugeuzwa Dampo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Serikali haitakubali Tanzania
kugeuzwa kuwa dampo la bidhaa za mifugo zilizokwisha muda wa matumizi na
kuua uwekezaji kwa manufaa ya watu wachache.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Saalam juzi, wakati wa kutoa matokeo ya
‘Operesheni Nzagamba’ iliyoendeshwa kwa vipindi viwili tofauti, Waziri
Mpina alisema kilo 26,295 za bidhaa za nyama na maziwa zimekamatwa,baada
ya kuingizwa nchini kutoka nje bila vibali, kulipiwa ushuru wala
kuhakikiwa ubora wake.
Pia
kilo 2,376 za bidhaa za nyama na maziwa yaliyokwisha muda wa matumizi
nazo zikikamatwa zikiuzwa maeneo mbalimbali na kuhatarisha afya za
walaji na kuingia katika hatari ya kupata magonjwa makubwa ikiwemo
saratani.
“Hatutakubali
kuua uwekezaji, viwanda na ajira za Watanzania kwa manufaa ya watu
wachache, hatutakubali kuziweka rehani afya za watanzania eti kwa sababu
ya uwekezaji operesheni hizi zitaendelea hadi pale wahalifu hao
watakapoacha mchezo huu mchafu,” alisema Mpina.
Alisema hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii kuliibuka taharuki juu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya wahalifu katika operesheni inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema
operesheni hiyo, inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria ina lengo la
kudhibiti uingizaji holela wa mazao ya mifugo nchini, kudhibiti uuzaji
wa mazao ya mifugo, pembejeo na chakula cha mifugo kilichokwisha muda wa
matumizi na utoroshaji wa mifugo na mazao yake nje ya nchi.
Alisema
kilo 17,712 za pembejeo za mifugo zilizokwisha muda wa matumizi
zilikamatwa, huku kilo 880 za nyama na maziwa ambazo hazina lebo wala
taarifa yoyote katika vifungashio pamoja na usajili kutoka mamlaka
husika nazo zikikamatwa.
Alisema
tani 25,423 za chakula cha mifugo zilikamatwa zikisafirishwa kwenda nje
ya nchi bila vibali ambapo katika uhakiki wa hesabu za ulipaji ushuru
kwa kampuni chache zilizofanyiwa uhakiki katika kipindi cha mwaka wa
fedha 2017/18, ilibainika Sh bilioni 4.25 zilikwepwa kulipwa
Alisema ng’ombe 40,954, mbuzi na kondoo 165,115 nazo
zilikamatwa
zikiwa zinatoroshwa kwenda nje ya nchi bila vibali na bila kulipa
ushuru wa aina yoyote huku zaidi ya ng’ombe 50,000 zilikamatwa zikiwa
zimeingia nchini bila vibali
Katika
operesheni hiyo,vifaranga 21,100 na mayai 21,480 yalikamatwa yakiingia
nchini bila vibali ambapo yalitaifi shwa na Serikali kisha kuketetezwa.
Alisema
licha ya bidhaa zinazoingizwa nchini bila vibali na huku Tanzania ikiwa
na mifugo mingi, uagizaji wa bidha za mifugo kutoka nje ya nchi ni
mkubwa nchini ambapo uagizaji wa bidhaa za nyama nchini umefi kia
thamani ya wastani wa sh. bilioni 10 huku maziwa ikiwa ni wastani wa sh
bilioni 30 kwa mwaka.
Waziri
Mpina ametaja baadhi ya madhara ya uingizaji holela wa bidhaa hizo
nchini ikiwemo kuathiri afya za wananchi kunakoweza kusababisha maradhi
sugu ikiwemo saratani.
Mpekuzi.
Comments