Kamandi ya kijeshi katika eneo la Kufra
huko Libya jana ilitangaza kuwa wanajeshi wa Libya wamefanikiwa
kulidhibiti kikamilifu eneo la kusini magharibi mwa nchi hiyo baada ya
kuwafurusha magaidi hao wa Daesh.
Kamandi hiyo ya kijeshi ya eneo la Kufra
imeongeza kuwa kundi la Daesh halina tena fursa ya kukariri
mashambulizi yake dhidi ya vijiji na vitongoji vinavyolindwa na jeshi la
Libya.
Mamluki wa kundi la kigaidi la Daesh hivi karibuni walikabiliana
na polisi wa Libya baada ya kufanya shambulio katika kituo kimoja cha
polisi kwenye mji wa Tazirbu wa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Katika mapigano hayo watu tisa wakiwemo
polisi watano waliuawa na kumi kujeruhiwa. Siku mbili zilizopita pia,
magaidi wa Daesh walionyesha picha wakidai kuwa wamewateka nyara karibu
watu 20 katika shambulio walilolifanya katika kituo hicho cha polisi.
Magaidi wa kundi la Daesh wamekuwa
wakifanya mashambulizi mengi katika miji ya kusini mwa Libya tangu
walipoanza kutorokea katika maeneo ya msituni nchini humo baada ya
kufurushwa katika mji wa bandari wa Sirte.
parstoday
Comments