WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema tayari imelipa malimbikizo ya walimu 700 kati ya walimu 719 waliokuwa wakidai Ungujana Pemba.
Malimbikizo hayo ni yale ya mishahara ya walimu wenye uzoefu wa miaka 30 kati kakazi.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mmanga Mjengo Mjawiri, aliyasema hayo wakati akizungumza na Zanzibar Leo ofisini kwake Mazizini.
Alisema walimu 19 ambao hawajalipwa kunatoka na matatizo ya kutoonekana majina yao wanaendelea na utaratibu wa kuwahakiki ili na wao walipwe stahiki zao.
Alisema, hivi sasa wizara ipo katika mchakato wa kuwalipa walimu 671 pesa likizo na posho kwa mwaka 2018 kwa utaratibu wa kawaida.
Alibainisha kuwa wakati wanaingia kuongoza wizara hiyo walikuta malimbikizo makubwa ya madeni ya walimu ambapo mpaka mwaka 2017 deni hilo lilikuwa limemelizwa.
Alisema, hatua hiyo imefikiwa kuhakikisha serikali inaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili walimu zikiwemo zinazohusiana na maslahi yao.
Hata hivyo, alibainisha kuwa katika kutatua changamoto ya upungufu wa walimu na wafanyakazi wizara tayari imeajiri wafanyakazi 1,114.
Hivyo, aliwaasa walimu kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa kufundisha kwa bidii.
Mbali na hayo alisema wizara itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili walimu ili waweze kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Zanzibarleo.
Comments