Serikali
imesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme
katika awamu ya tatu ya mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (Rea).
Aidha,
Serikali imetenga Sh1 trilioni kwa ajili ya kusambaza umeme katika
vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati hiyo huku
ikiendela na uwekaji wa umeme katika vijiji zaidi ya 13400.
Mbunge
wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga amewahakikishia
wananchi kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo hilo hivyo wananchi
wanapaswa kuondoa wasiwasi na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Mhe
Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano yake katika kijiji cha Igale
na Iyula A vilivyopo katika kata ya Iyula akiwa katika ziara ya kikazi
jimboni humo.
Alisema
kuwa upatikanaji wa umeme katika jimbo lake utasaidia kuongeza
upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kuwa chachu ya maendeleo
kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema
kuwa utekelezaji wa Miradi hiyo ya umeme katika Jimbo la Vwawa unaenda
sambamba na lengo la Serikali ya awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati
kupitia viwanda ifikapo 2025.
Mhe
Hasunga amewataka wananchi hao kutumia fursa mbalimbali zitakazotokana
na utekelezaji wa miradi katika sekta ya gesi na mafuta ili kujiongezea
kipato na kuiwezesha nchi kutimiza malengo yake kuelekea kuwa nchi ya
uchumi wa kati.
Kuhusu
malalamiko ya wananchi dhidi ya gharama kubwa za pembejeo za kilimo,
Mhe Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo amewahakikishia wananchi kuwa
wizara yake imejipanga kuhakikisha kuwa mbolea zinapatikana kwa wakati
ili wakulima wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara waweze kunufaika
na pembejeo hizo.
Alisema
kuwa kumekuwa na malalamiko mengi nay a muda mrefu kuhusu mbolea hivyo
serikali itapitia upya utaratibu wa uuzaji wa mbolea ili kutafuta namna
bora ya kurahisisha huduma hiyo kwa wakulima nchini.
Mpekuzi.
Comments