Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutarifa umma kuwa leo
tarehe 19/12/2018, itafunga kwa muda barabara ya Morogoro sehemu ya
Kimara Stop Over hadi Temboni Wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam
kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.
Kufungwa
kwa muda barabara hii kunatokana na kuwepo kwa sherehe ya uwekaji wa
jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa
19.2 kutoka Kimara hadi Kibaha kuwa njia nane (8) itakayofanyika eneo
la Kimara Stop Over.
Wizara
inashauri watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara mbadala kwa muda
wote ambao barabara hiyo itakuwa imefungwa kwa muda.
Aidha, Wizara inawaomba radhi watumiaji wote wa barabara hiyo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Comments