Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, amelitaka Shirika la
Madini la Taifa (Stamico) kutumia mtambo wa kuchoronga miamba kwa
ufanisi ili kuliletea tija taifa.
Prof.
Msanjila aliyasema hayo juzi wakati wa hafla fupi ya kuukabidhi rasmi
mtambo huo kwa Stamico kwa ajili ya kuanza kuutumia rasmi.
Alisema
ununuzi wa mtambo huo ni uwekezaji mkubwa ambao serikali imeufanya kwa
Stamico, hivyo shirika hilo halina budi kuutumia vyema ili kuleta tija.
Kuhusu
gharama za mtambo huo, Prof. Msanjila, alisema umegharimu Dola za
Kimarekani milioni 1.3, ambazo akiwa mtendaji mkuu wa wizara anaona ni
deni kubwa kwake, hivyo kuahidi kuusimamia ipasavyo ili kuhakikisha
unazalisha faida na kuwa chachu ya kununua mitambo mingine kama hiyo ili
kukuza sekta ya madini nchini.
Pia
alilitaka shirika hilo kujitangaza vyema ili wananchi, hususan wadau wa
madini wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na utafutaji, kufahamu
uwepo wa mtambo huo ili utumike hata kwa kampuni binafsi ili kujiongezea
kipato na pia kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini.
“Kwa zabuni nilizozisikia mpaka sasa mtambo huu utazalisha pesa za kutosha,” alisema.
Prof.
Msanjila pia aliitaka Stamico kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi
ya mtambo huo kila robo ya mwaka, ili kufanya tathmini endapo mtambo
unatumika kwa faida.
Pia
aliliagiza shirika hilo kuhakikisha mtambo huo unawezesha ununuzi wa
mtambo mwingine mpya kila mwaka, ili ndani ya miaka mitano shirika
limiliki mitambo mitano na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za
uchimbaji na utafutaji wa madini.
Mpekuzi.
Comments