Umoja
wa Wataalam Wasaidizi Tanzania (TAVEPA), umeiomba Serikali kuweka
mkakati wa makusudi wa kunusuru zao la ngozi kwa kuwa sasa hivi hakuna
soko la uhakika la zao hilo.
Mwenyekiti
wa (TAVEPA) Bw. Salim Msellem, alisema hayo jana (03.12.2018) Jijini
Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa wataalam wasaidizi wa afya
ya mifugo nchini.
“Ngozi
nyingi hutupwa, kitu ambacho kinaletea hasara taifa kwa kukosa fedha za
kigeni, pia kudhoofisha uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja wa ngozi
hapa nchini,” alisema Bw. Msellem.
Alisema
pia lazima kuwe na mkakati wa dhati wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo
vya kuchakata ngozi utasaidia kunusuru zao la ngozi.
Akizungumzia
uwezo mdogo wa wahitimu wa stashahada ya afya na uzalishaji mifugo
(DAHP), alisema, TAVEPA imepata malalamiko toka maeneo mbalimbali ya
nchi kuhusu suala hilo.
“Wahitimu
wa DAHP imebainika muda wa mwaka mmoja wa masomo ya stashahada ya afya
ya Mifugo (DAHP) hautoshi, ombi letu tunaomba stashahada iwe kama awali,
ya miaka miwili au miaka mitatu na msisitizo uwe mafunzo kwa vitendo
ili kumuandaa mhitimu kufanya kazi kwa ufanisi kama ilivyokuwa miaka ya
nyuma.
“Kwa
sasa inaonekana wanasoma kwa ajili ya kwenda vyuo vikuu na siyo kwenda
kuwasaidia wafugaji kule vijijini, hakika uwezo wao kwa vitendo ni mdogo
sana,” alisema Bw. Msellem.
Aidha
umoja huo umeiomba serikali kuandaa mkakati wa dhati wa kusimamia
mafunzo rejea kwenye tiba, matumizi sahihi ya dawa, ukaguzi wa vyama,
ubora wa ngozi na ubora wa wanyama wanaotaka kuchinjwa kwa watumishi wa
umma na sekta binafsi mara kwa mara ili kuwajengea uwezo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Madaktari wa Mifugo (TVA), Prof. Dominic Kambarage,
alisema Tanzania ina ng'ombe wengi na inauza ng'ombe hizo nchi
mbalimbali za Afrika Mashariki hivyo ni vyema wafugaji wakachangamkia
Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Prof.
Kambarage alisema ni vyema sasa wafugaji wakapewa elimu ya kutosha
pamoja na upatikanaji wa chanjo za mifugo ili kudhibiti magonjwa pamoja
na kupata masoko ya uhakika ili kila mtu anufaike na rasilimali hiyo.
"Sekta
ya mifugo ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi na Tanzania ni ya
pili Barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi, hivyo mifugo hiyo ikitumika
vyema itasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuongeza kipato, "
alisema.
Naye
Msajili wa Baraza la Veterinari (VCT) nchini, Dkt. Bedan Masuruli,
alisema ni vyema kudhibiti magonjwa yatokanayo na mifugo kwani asilimia
70 ya magonjwa ya kupe yanaua mifugo hivyo ni vyema wafugaji wakaogesha
mara kwa mara mifugo yao ili kudhibiti ugonjwa wa kupe.
Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Mpekuzi.
Comments