Rais
John Magufuli amesema waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi wa barabara
ya Morogoro eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaam hawatalipwa
fidia kwa kuwa walijenga katika eneo la hifadhi ya barabara.
Rais
Magufuli ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika
hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo inayofanyika
eneo la Kimara Stop Over.
Huku akirejea mara tatu kusema "hakuna fidia", Magufuli amesema hata wakienda mahakamani hakuna fidia.
“Niwambie
tu wananchi kuwa ukisogelea barabara madhara yake ni umasikini, hata
mimi sijafurahishwa na hii bomoabomoa kwa kuwa wapo ndugu zangu nyumba
zao zimebomolewa,” amesema.
"Ni vyema kuwaambia ukweli kesi hii hata wakienda wapi hawawezi kushinda."
Comments