Mkazi
wa Kijiji cha Nakayaya, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Awetu Makunula
(44), amejinyonga hadi kufa kwa madai ya kuchoka kusumbua wanafamilia
kutokana na hali ya afya yake.
Taarifa
za tukio hilo zinaeleza kuwa Makunula alikutwa akining`inia juu ya mti
wa mkorosho jirani na nyumba ya wazazi wake, mjini hapa.
Mume
wa marehemu Makunula, Salum Namtikwe, alisema kuwa usiku walilala wote
na kabla ya tukio hilo aliamka majira ya saa 11 alfajiri na kumuaga kuwa
anatoka nje kwa ajili ya kufagia nje ya nyumba yao ili amalize shughuli
hiyo mapema na kwenda shambani.
Alisema
baada ya kupewa maelezo hayo yeye aliendelea kulala, lakini baadaye
alishangaa kupata taarifa za mkewe kukutwa akiwa amejinyonga hadi kufa
baada ya kujining`iniza katika mti uliopo jirani na nyumbani kwa wazazi
wake.
Alisema
baada ya kupatiwa taarifa hizo aliamka na kwenda eneo la tukio na
kumtambua marehemu na baadaye walitoa taarifa kwa viongozi wa serikali
kwa ajili ya taratibu za kuuondoa mwili huo katika eneo hilo.
Aidha,
akisimulia maisha ya mkewe, alisema kabla ya tukio hilo alikuwa
akisumbulia na maradhi mbalimbali mara kwa mara jambo ambalo lilikuwa
likimnyima amani wakati wote.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, ASCP Gemin Mushy, alithibitisha kuwapo kwa
tukio hilo na kusema polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo
cha kifo hicho.
Kamanda
Mushy, alisema katika tukio hilo mwanamke huyo alijinyonga kwa kutumia
mtandio alio jifunga shingoni na upande mwingine kuufunga juu ya mti wa
mkorosho.
Mpekuzi.
Comments