Watu
wawili wanaodaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi, Karoli Domisian
(36) na Regina Temu (29) wamefariki katika mtaa wa Mafumbo, manispaa ya
Bukoba mkoani Kagera baada ya mwanaume kumuua mpenzi wake kisha yeye
mwenyewe kujinyonga, kisa usaliti wa mapenzi.
Kamanda
wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kwamba mauaji hayo yamegundulika Desemba 17 saa 11
jioni katika mtaa huo.
Amesema
kuwa Regina Temu (29) ambaye ni mkazi wa Kahororo katika manispaa hiyo
na mfanyakazi wa kiwanda cha kusindika kahawa cha Tanica alikutwa
amenyongwa kwa tai nyumbani kwa Karoli Domisian (36), Mwalimu wa shule
ya sekondari Nyanshenye iliyoko katika Manispaa ya Bukoba, ambapo baada
tu ya kutekeleza mauaji hayo, Karoli alijinyonga palepale kwa kutumia
kamba ya manila ndani ya chumba chake.
"Ndani
ya chumba chake kulikutwa karatasi yenye ujumbe wa maandishi
iliyoonekana kuandikwa na mwanaume, kwamba amejinyonga mwenyewe baada ya
kumuua mpenzi wake, kutokana na kumsaliti"Kamanda Malimi.
Malimi
ameeleza kwamba Regina alikuwa akiishi na dada yake eneo la Kahororo na
kuwa aliondoka Desemba 16 mwaka huu saa kumi jioni na kuaga kuwa
anakwenda sokoni lakini hakurudi nyumbani.
"Baada
ya dada yake kuona hakurudi, kesho yake ambayo ni Desemba 17, 2018
alianza kumtafuta hadi polisi bila mafanikio, lakini ilipofika saa 11:30
jioni aliamua kuongozana na mtu mwingine kwenda kwa hawara wa mdogo
wake na baada ya kufika huko ndipo aligundua kuwa mdogo wake ameuawa na
kutoa taarifa polisi ambao waliwahi kufika katika eneo la tukio na
kukuta marehemu hao na karatasi yenye maandishi hayo".
Kwa mujibu wa kamanda huyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo.
Mpekuzi.
Comments