Kutokana
na kina cha bahari ya Hindi katika eneo la Mnazi Bay Msimbati mkoani
Mtwara kuendelea kumomonyoka siku hadi siku kuelekea nchi kavu, huenda
nchi ikajikuta gizani kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Hayo
yamesemwa jana Jumatatu Desemba 4, 2018 na Naibu mkurugenzi wa Kampuni
ya Maurel & Prom Tanzania inayohusika na kuchimba gesi, Elias
Kilembe kwa Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alipotembelea visima
hivyo vya gesi.
Kilembe
alisema siku hadi siku bahari inasogea nchi kavu kuelekea kilipo moja
ya kisima cha gesi na mitambo hali inayowapa wasiwasi.
“Hata
mwaka jana ulitokea mmomonyoko lakini haukuwa tishio kama wa mwaka
2015, lakini ukija hapa baharini unakuta mchanga umeondoka wote na
kupotea, kweli ni tishio kwa kambi hii,” alisema Kilembe.
Waziri
wa nishati, Dk Kalemani amesema hali halisi inaonekana na hakuna haja
ya utafiti, bali kinachotakiwa kufanyika ni kujengwa kwa ukuta haraka
ambao utatenganisha kisima kilipo na bahari ili kuepuka athari
zinazoweza kujitokeza.
“Kuanzia
sasa anzeni kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika
mahala mtakosa hata pa kuweka ukuta maji yakishafika huku, ni vizuri
kuanza sasa ili msije kukumbwa na dhoruba kubwa, haya ni maagizo ya
haraka haraka wala si jambo la kufanya utafiti,” amesema Dk Kalemani.
Mpekuzi.
Comments