Jeshi
la Polisi Jijini Dodoma linaendelea na misako katika maeneo mbalimbali
ya jiji hilo ambapo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 64 wakiwemo Wezi,
Makahaba na Wauza Madawa ya kulevya.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu kukamatwa kwa
watuhumiwa 64 kati yao wakiwamo 11 wa ukahaba, Kamanda wa Polisi mkoani
humo, Gilles Muroto, alisema kuwa jeshi hilo litaendelea kuwakamata watu
hao kwa kuwa wanachafua taswira ya jiji hilo.
Kamata
kamata ya watu wanaofanya biashara hiyo, ilianza Oktoba 9, mwaka huu na
kukamata makahaba 22, wanaume watano waliokuwa wakiwanunua pamoja na
wamiliki wanne wa maeneo yanayoruhusu biashara hizo.
Aidha, Oktoba 31, mwaka huu, jeshi hilo liliwakamata watu wengine 17 wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.
"Watuhumiwa
hawa wote watafikishwa mahakamani na jeshi letu litaendelea na msako wa
kuwakamata makahaba wote jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa ndiye
balozi wetu wa kupinga maambukizi mapya ya Ukimwi,hivyo hatuwezi
kuendelea kuwavumilia hawa watu," alisema Muroto.
Alisema
kumekuwa na ongezeko la biashara hiyo kwa kasi, hivyo ni vyema watu
wakachukua tahadhari kujiepusha na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa
huo.
Alisema kuwa watuhumiwa hao wote wamekamatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo katika maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa msako huo ulihusisha pia ukamataji wa mali za wizi na wapokea mali hizo pamoja na wavunjaji wa nyumba za watu na kuiba.
Alisema kuwa msako huo ulihusisha pia ukamataji wa mali za wizi na wapokea mali hizo pamoja na wavunjaji wa nyumba za watu na kuiba.
Katika
tukio jingine, Muroto alisema wamekamatwa watuhumiwa sita na dawa za
kulevya aina ya bangi misokoto 420 ya majani ya bangi, pamoja na kilo
tatu za majani ya bangi kinyume cha sheria.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Christopher Edward (25), mkazi wa Chang'ombe,
Hafidhu Mohamed (32), mkazi wa Ntyuka na Cosmas Ndalu, mkazi wa Maili
Mbili.
Pia walikamatwa watuhumiwa wengine watatu Asha Omary, mkazi wa Chamwino, Tatu Shabani na Ashirafu Hassan, wakazi wa Chang'ombe wakiwa na pombe haramu ya gongo.
Pia walikamatwa watuhumiwa wengine watatu Asha Omary, mkazi wa Chamwino, Tatu Shabani na Ashirafu Hassan, wakazi wa Chang'ombe wakiwa na pombe haramu ya gongo.
Muroto
aliongeza kuwa jeshi hilo limemkamata Mkazi wa Chamwino Msafiri
Stephano (32) akiwa na mafuta aina ya dizeli lita 100 zinazodaiwa kuwa
za wizi.
Katika tukio jingine wamekamatwa watuhumiwa saba kwa makosa ya kuvunja na kuiba wakiwa na mali za wizi mbalimbali
Kadhalika, Muroto aliwataka wananchi wa mkoa huo katika kipindi hiki cha sikukuu kila mtu achukue tahadhali za kuhakikisha usalama katika maeneo yao.
Kadhalika, Muroto aliwataka wananchi wa mkoa huo katika kipindi hiki cha sikukuu kila mtu achukue tahadhali za kuhakikisha usalama katika maeneo yao.
mpekuzi.
Comments