Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania
kuhusu matokeo ya uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 47 Tanzania
Bara uliyofanyika tarehe 02 Desemba 2018 na kwamba CCM imepita bila
kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi CCM
imeshinda kwa kishindo.
Katika
chaguzi hizi ambazo CCM imeendelea kuongoza inajivunia umakini mzuri wa
kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria za Nchi yetu, Sera nzuri, ahadi
zinazotekeleka na siasa safi na uongozi bora.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwashukuru watanzania na wanaCCM wote
kwa kuendelea kukiamini na kukichagua na kwamba CCM itaendelea
kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa
haraka katika maeneo yao.
Aidha
Chama kinapenda kuwafahamisha kuwa tarehe 17 hadi tarehe 18 Desemba
2018 Jijini Dar es salaam kutakuwa na vikao vya Chama vya kawaida vya
Uongozi Taifa ambapo tarehe 17 Desemba 2018 kutakuwa na Kikao cha Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na tarehe 18 Desemba 2018 Kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa kitaketi. Hivyo taarifa hii inawajulisha
wajumbe wote wa vikao husika kufika katika vikao hivyo.
CCM
inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea
kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Ndg. Bashiru Ally
Katibu Mkuu wa CCM kwa Ndg. Benard Membe ambaye ni Mwanachama wa CCM
kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na Viongozi
na Wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa
wanaCCM.
Tunapenda
kutoa rai kwa watanzania kuwa wito wa Katibu Mkuu ulikuwa ni wito wa
kawaida wa Kiongozi wa CCM kwa mwanachama wa CCM, hivyo uzushi,
uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea hasa katika
mitandao ya kijamii na baadhi ya Magazeti yenye hila mbaya, wana CCM na
Umma wa watanzania wanaombwa waupuuze.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinawataka wana CCM na watanzania kwa ujumla
kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo zaidi katika kipindi hiki
ambacho Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anandelea kutuongoza katika Mageuzi
makubwa ya kiuchumi na ya kimaendeleo kwa watanzania wote.
Mpekuzi.
Comments