Zaidi Ya Bilioni Tatu Zatafunwa......waziri Mkuu Aagiza Kuchukuliwa Hatua Kwa Watumishi Wote Waliohusika.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya
ya Nyangw’ale waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu
fedha ambazo zilitolewa na Serikali kugharamia miradi ya maendeleo
wachukuliwe hatua.
Pia
ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa Mkaguzi wa Ndani wa
halmashauri hiyo, Gavana Matesa kwa sababu ameshindwa kutoa kwa mamlaka
husika kuhusu taarifa za wizi wa fedha za maendeleo zilizotafunwa.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo jana (Jumatano, Novemba 28, 2018) wakati
akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale akiwa
katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Geita.
Miongoni
mwa miradi ambayo fedha zake zimepotea ni pamoja na sh. bilioni 1.2 za
ujenzi ofisi ya halmashauri hiyo, sh. milioni 400 za ukarabati wa kituo
cha afya Nyangw’ale, sh. milioni 611.230 za miradi ya maji.
Nyingine
ni sh. milioni 536.119 za mpango wa malipo kulingana na huduma (EP4R),
sh. milioni 125.914 za ushuru wa huduma, sh. milioni 31 za ujenzi wa
ofisi ya mbunge na sh. milioni 109 za mfuko wa barabara.
“Wilaya
ya Nyangw’ale ni mpya na Serikali imekuwa ikileta fedha nyingi lakini
fedha zote zimetafunwa, Serikali ipo makini sana na moja kati ya vita
kubwa ni dhidi ya mafisadi, wala rushwa ambayo ni endelevu hivyo
tutashughulika na kila mmoja.
Tayari
watu saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya ya Nyangw’ale, Carlos Gwamagobe na wenzake wamekamatwa. Wizi
unatisha Nyangw’ale wilaya inatia aibu tutawaondoa watu wote waliohusika
na tutaendelea kuwakamata.”
Hata
hivyo Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba
Serikali itahakikisha miradi yote iliyoahidiwa kujengwa kwenye wilaya
hiyo ikiwemo ya maji itatekelezwa kama ilivyopangwa, waendelee kuwa na
imani na Serikali yao.
Kuhusua
suala la watumishi, amesema wilaya hiyo lazima iwe na watumishi wasafi
wenye weledi wa kufanya kazi na lazima wahakikishe fedha za miradi
zinazotolewa katika halmashauri hiyo zinalingana na thamani halisi ya
mradi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema
atahakikisha watumishi wote wa umma waliohusika na wizi huo
wanachukuliwa hatua stahili na kwamba tayari baadhi yao wameshafikishwa
kwenye vyombo vya dola.
Amesema
halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale inaongoza kwa matumizi mabaya ya
fedha za maendeleo kwa kuwa awali lilikuwa chaka kubwa la wizi, ambapo
amesema ni bora watumishi wote wasiokuwa waadifu waondolewe na waletwe
wengine.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel amesema tayari baadhi ya
watumishi wanaotuhumiwa kuhusika katika ubadhilifu wa fedha za miradi
mbalimbali wameshakabidhiwa kwa vyombo vya dola huku watumishi wengine
wakiendelea kuchunguzwa.”Watumishi wote waliohusika na wizi huu watapata
tabu sana”
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
Mpekuzi.
Comments