Akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa kesi za rushwa
zipo na zinazohusiana na michezo Zanzibar, lakini kutokana na michezo
inavyo chezwa jamii bado haijawa na mwamko wa kuzitolea taarifa.
Alisema kuwa hii inatokana na kwamba wanamichezo hao walikuwa
hawajui kwamba rushwa inahusika pia katika michezo na kuamini na
inaingia katika kuhujumu uchumi.
Hata hivyo alisema kuwa mpaka sasa wanazo kesi chache zinazohusiana na rushwa michezoni ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi.
Samabamba na hilo alisema kuwa baada ya kuona hivyo waliamua kufanya
mafunzo ya kuwaelimisha kwa kuandaa mkutano maalumu na kuwashirikisha
wanamichezo wakiwemo viongozi, waamuzi na wote wanaohusiana na michezo.
Hivyo alisema kuwa mafunzo hayo yameweza kutoa mwamko na kujua
kwamba na wao wana haki au uwezo wa kutambuwa kwamba hichi
kinachofanyika katika michezo ni rushwa na wanaweza kukiripoti.
Hata hivyo alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikizidi kuwashajiisha
na kushukuru kushirikishwa katika mambo mbali mbali wanayofanya katika
kuimarisha michezo .
Zanzibarleo.
Comments