Siku
chache baada ya Benki kuu ya Tanzania kutoa ufafanuzi Juu ya Oparesheni
ya Ukaguzi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Jijini Arusha
,Wizara ya Mali asili na Utalii imejitokeza na kusema Zoezi hilo
halijaathiri shughuli za Kitalii
Naibu
waziri wa maliasili na Utalii Constatine Kanyasu ameyasema hayo wakati
lipotembelea taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwenye mkutano wake
na wafanyakazi wa shirika la hifadhi za taifa(TANAPA) jijini Arusha na
kusema watalii wanaendelea kupata huduma kwani zoezi hilo ni la kawaida
na limelenga maslahi ya nchi.
Mara
baada ya Mazungumzo hayo Naibu Waziri akiwa nje ya Ukumbi wa Mamlaka
hiyo , amezungumza na Wanahabari kisha kugusia suala la oparesheni
iliyofanywa na Benki Kuu hivi karibu Jijini hapa.Ameeleza kuwa zoezi
hilo lililovishirikisha vyombo vya dola na halijaathiri uchumi katika
sekta ya fedha za kigeni hasa kwa upande wa utalii kwa kuwa ni zoezi
hilo la mara moja kuwahusisha wanajeshi ambao wanawajibu wa kulinda
rasilimali za nchi yao.
''
Wanajeshi hawawezi kuathiri uchumi wa nchi hasa sekta ya utalii kwakuwa
wanawajibu wa kulinda rasilimali zetu‘’alisema Kanyasu .Akiongelea
suala la migogoro ya Ardhi na mipaka kwa baadhi ya mipaka amesema wizara
yake imejipanga kukomesha changamoto hiyo ambayo imekuwa ikitumia fedha
nyingi bila kupatiwa ufumbuzi.
Aidha
amesema migogoro baina ya Hifadhi na Wananchi,Naibu waziri anasema
hakuna mtu ama taasisi inayonufaidika na Migogro hiyo na imekuwa
ikichochewa na makundi machache na tayari serikali imekwisha anza
kuchukua hatua.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Jumla ya Vijiji
mia tatu tisini na mbili vitanufaika na zoezi la upimaji wa matumizi
bora ya ardhi lenye lengo la Kupunguza
Migogoro
ambapo tumepanga billion 2.5 kwa miradi midogo midogo kuweza kuweka
nguvu kwa wananchi kuondoa misuguano isiyo na lazima ambayo inaathiri
kiasi kikubwa shughuli za uhifadhi.
Mpekuzi.
Comments