
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Singu wilaya ya Babati mkoani Manyara Lukuvi
alisema uamuzi wowote wa kupima viwanja unatakiwa kuratibiwa na
halmashauri husika kwa kuzingatia mipango miji na si vinginevyo kwa kuwa
mwenye dhamana ya kupanga miji ni halmashauri.
Agizo
la Waziri Lukuvi linafuatia kuelezwa na halmashauri za wilaya ya Babati
kuhusu mpango wa kupima viwanja katika eneo la shamba la Singu Estate
linalomilikiwa na kampuni ya Agric Evolution Ltd .
Lukuvi
ameziagiza halmshauri za Mji na ile ya wilaya ya Babati kuainisha
mipaka na kupima eneo la vijiji vya Singu, Sigino na Daglailoy vilivyopo
kata ya Singu wilaya ya Babati sambamba na kuvipatia hati vijiji vyote
na kubainisha kuwa zoezi la kugawa viwanja katika shamba linalomilikiwa
na kampuni ya Agric Evolution ltd litafanyika baadaye kwa utaratibu
utakaopangwa.
Lukuvi
alisema ameamua kusitisha ugawaji viwanja baada ya kubaini ukiukwaji wa
taratibu sambamba na baadhi ya wawekezaji kununua mashamba katika
maeneo ya mjini kwa nia ya kuzishawishi halmshauri kupima viwanja badala
ya halmashauri kupima kulingana na mipango yake.
”
kumekuwa na mtindo wamiliki wa mashamba wanachukua maeneo ambayo
wanaona yanakaribia kuwa miji kwa lengo la kupima viwanja na
kuwalambisha asali watendaji wa halmashauri ili malengo yao yatimie”
alisema Lukuvi.
Aidha,
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi william Lukuvi ameagiza
wananchi 14 waliojenga katika shamba la Endasago lililopo kata ya Ari
wilaya ya Babati mkoa wa Manyara unapopita mradi mkubwa wa umeme Kilowat
400 kulipwa fidia na kuondoka eneo hilo.
Uamuzi
wa kulipa fidia kwa wananchi hao unatoa suluhu ya muda mrefu baina ya
mmiliki wa shamba kampuni ya Endasago co ltd na wananchi waliojenga
katika njia ya kupitisha umeme wa mkongo kutoka Singida kupitia Babati,
Namanga mpaka Kenya huku utata ukiwa ni nani anastahili kulipwa fidia
kati ya pande hizo mbili.
Amelitaka
shirika la Umeme tanesco kuendelea na zoezi la kuweka nguzo kwa ajili
ya kukamilisha upitishaji nyaya za umeme katika mashamba yote mawili ya
Endasago na Singu lakini malipo ya fidia yatakuwa kwa wale wananchi wa
kijiji cha Endasago pekee.
“Tanesco
muendelee na uwekaji nguzo katika mashamba yote mawili na wananchi
wasimame kufanya shughuli yoyote wakati wa zoezi hilo.
Pamoja
na uamuzi wa fidia, Lukuvi ameitaka halmashauri ya wilaya ya Babati
kupima upya eneo la shamba la Endasago na kumpatia mmiliki wake eneo
kulingana na mahitaji yake. Aidha, alimuagiza mmoja wa wana hisa wa
Kampuni ya Endasago Abraham Mchinja kufuatilia hati ya shamba pamoja na
kuhuisha umiliki wa kampuni ya Endasago co Ltd ambayo wanahisa wake
wawili wamefariki dunia na kubaki mmoja pekee.
Mbunge
wa jimbo la Babati Paulina Gekul aliiomba serikali kuangalia namna ya
kuwasaidia wananchi wa vijiji vya Endasago na Singu dhidi ya wamiliki wa
mashamba hayo mawili kwa kuwa wananchi wa vijiji hivyo wamekuwa
wakiishi eneo hilo kwa muda.
Kwa
muda mrefu kumekuwa na mgogoro mkubwa baina ya wananchi wa vijiji vya
Singu, Sigino na Daglailoy vilivyopo kata ya Singu na vile vya Endasago
na Dudiye vilivyopo kata ya Ari wilayani Babati na wamiliki wa mashamba
ya Endasago lenye ukubwa wa 1300 na Singu ekari 3013 kuhusiana na
umiliki wa mashamba.
Mpekuzi.
Comments