Idadi hiyo ni wastani wa watoto 50 kwa mwezi, kiwango ambacho ni kikubwa.
Aidha idadi ya watoto wanaozaliwa kwa siku katika hospitali hiyo wanafikia 70-100 kutokana na wazazi wengi kukimbilia kujifungua katika hospitali hiyo.
Muuguzi mkunga katika wodi ya watoto wachanga na watoto njiti katika hospitali hiyo, Salama Ame Bakari, aliyasema hayo wakati akizungumza na gazeti hili, Mnazimmoja.
Alisema kuna sababu mbali mbali zinazopeleka mama mjamzito kujifungua mtoto njito ikiwemo msongo wa mawazo wakati wa ujauzito na mama kutopata matunzo mazuri.
“Wapo wanawake ambao hupata msongo wa mawazo hali inayosababisha kujifungua kabla ya wakati lakini pia tatizo la matunzo duni nalo linachangia wajawazito kujifungua watoto njiti,” alisema.
“Kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa akiwa na uzito wa kilo 2.3 na anapozaliwa na uzito wa kilo 1.2 anatakiwa kuwekwa kwenye uangalizi maalumu wa daktari hadi atimize uzito wa kilo 1.8 hapo ndipo anapewa mzazi kwenda kumlea mwenyewe nyumbani,” alisema.
Alitaja sababu nyengine ya kuzaliwa watoto njiti ni mwanamke kubeba mimba yenye watoto zaidi ya mmoja, kufanya kazi ngumu wakati wa ujauzito, ulevi na mwanamke kubeba ujauzito chini ya umri wa miaka 18.
Aliwaomba wanaume kuwa karibu na wenza wao wakati wa ujauzito ili wapate utulivu na kuhakikisha wanawapatia vyakula vinavyojenga afya.
Zanzibarleo.
Comments