
Baraza la Wauguzi lina sheria zake kwa wafanya kazi wake kwanza
kuitumikia dhamana alopewa na kuithamini kazi yake wakat wa kutoa huduma
kwa wagonjwa wao kwani wanaonekana ndio masuli wa kila jambo linalotokea
kulifahamu .
Kauli hiyo imetolewa na msaidiz Mrajis wa baraza la Wauguzi Pemba
Sabra Salum Suleiman ,wakati alipokuwa akizungumza na Wauguzi na Wakunga hapo
hospitali ya Chake chake katika kukumbusha umuhimu wa utendaji kazi
wao kwani ni watu muhimu kwa jamii kutokana na kazi zao.
Alifahamisha kwamba asilimia 50 ya wafanyakazi ni Wauguzi hivyo
wanatakiwa kujitambua na kuwa na madili mazuri na kutumia lugha nzuri na upole
wakati wanapotoa huduma kwa wagonjwa walolazwa na wanaokwenda na kurudi.
“Nakuombeni wafanya kazi wezangu fanyeni kazi kwa kuguata sheria
ya mabaraza ya Uuguzi unavyoelekeza na mtu kujua majukumu yake niyepi”.alisema
Msaidizi Mrajisi huyo.
Alifahamisha kuwa mfanya kazi yoyote anatakiwa kufanya kazi kwa
wakati uliopangwa ambao ni saa moja na robo wanatakiwa kukabidhiana ofisi na
kwa maandishi kutoka kwa mtu wazamu alokuwepo kazini usiku.
Aidha alisema kwa watu wanaoingia kazini mchana wanatakiwa kufika
kazini saa saba na nusu ili kuweza kukabidhiana zamu zao na kumkabidhi wagonjwa
ambao wanahudumiwa na kupita Wodi moja moja kuwaona wagonjwa ambao wamelazwa
ili iwe rahis kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake Afisa Muguzi Msaidiz Pemba Dr
Omar Juma Ali ,alisema baraza la Wauguzi kupitia Sheria namba 5 ya mwaka 2014
ambayo imepitishwa na baraza la Wawakilishi imeleza mambo mengi ikiwemo
uwajibikaji wa kufanya kazi kwa uwadilifu pamoja na makosa na adhabu zake iwapo
atatenda kinyume na kanuni za utumishi.
Hata hivyo aliwaomba wauguz hao na wakunga kuweka utaratibu wa
kufanya vikao kila miezi mitatu kujadili changamoto za kiutendaji ili
kuweza kuzitatua kwa uwongozi wa chini kabla ya kufika uwongozi wa juu.
“Utaratibu wa kazi unahimiza kwamba kila miezi mitatu kunatakiwa
kufanyike vikao ambavyo vitajadili changamoto na kuhimizana uwajibikaji wa kazi
kwa kila mfanyakazi juu ya majukumu yake”.
Akielezea suala la leseni kwa wauguzi hao alisema ni jambo la
muhimu sana kwanza linamtambulisha kujulikana na yule anaetaka kumfanyia huduma
ili iwe rashis kwake kutoa huduma.
Hata hivyo alifahamisha kwamba faida ya kuwa na lesini
inakupunguzia matatizo na gharama kwani hapo awali bei ya kawaida ilikuwa
40,000 na sasa 50,000 ambapo bei hiyo ni kwa muda na itarejea
kama ya awali na ilopita muda ya kurinyuu ni 50,000 .
Nao wauguzi hao wamewahidi viongozi wao kuyafanyia kazi maagizo
walipewa ili kuona mabadiliko yanaongezeka zaid ya utendaji kazi na kutoa
huduma kwa wananchi wao.
Comments