Wahasibu watakiwa kusimamia fedha za umma.

Image result for mkuu wa mkoa wa kusini PembaMKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, amewataka wahasibu na wasimamizi wa idara, kuzisoma na kuijua sheria ya usimamizi wa fedha namba 12 ya 2016.
Alisema haipendezi kuona wakuu wa idara na wahasibu, hawaifahamu sheria hiyo hali inayosababisha serikali kukosa mapato yake.
Aliyaeleza hayo katika ukumbi wa ZSSF, Chake Chake, wakati akifungua mafunzo ya sheria ya usimamizi wa sheria ya fedha namba 12 ya 2016, kwa wakuu wa mikoa, wilaya, Makatibu tawala mikoa na wilaya, maofisa wadhamini, wahasibu na wakaguzi wa hesabu.
Alisema utekelezaji wa mageuzi katika mifumo ya usimamizi wa fedha umerahisishwa ili kuondoa udanganyifu katika masuala ya fedha.
“Zanzibar sio ya kwanza kuanza kufuata mfumo huu wa mageuzi ya fedha, nchi kama Afrika Kusini na Mauritius zimeanza zamani na mafanikio yanaonekana,”aliongeza.
Aidha aliwataka wahasibu kuhakikisha wanasimamia fedha katika taasisi zao na kuziwasilisha kunakohusika kwa wakati.
Ofisa Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango, Ibrahim Saleh Juma, alisema wizara itaendelea kusimamia suala la kodi ili kuimarisha maendeleo.
Akiwasilisha mada ya ijue hazina ya serikali, Mhasibu Mkuu wa serikali, Mwanahija Almas Ali, alisema sheria imefanyiwa mabadiliko makubwa na haikuacha kitu ili iweze kwenda na wakati katika usimamizi wa fedha.
Akiwasalisha mada juu ya usimamizi wa fedha kwa mashirika ya umma, Muhasibu, Ame Burhan Shadhil, aliwataka wahasibu wa serikali za mitaa,
Zanzibarleo.

Comments