Mbunge
wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, amebainisha matumizi ya
pesa zake anazoingiza kwenye muziki amekuwa akizitumia katika
kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo yatima.
Sugu
ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini kwa muhula wa pili, amebainisha hayo
wakati akimjibu moja ya wafuasi wake kupitia akaunti yake Instagram.
Katika
chapisho hilo la Joseph Mbilinyi moja ya wafuasi wake aliyesomeka kwa
jina la Emmanuel Syonga aliandika “Mbeya wanahitaji huduma za jamii sio
tamasha.”
Akijibu
Swali hilo Mbunge huyo aliandika ;“toka niwe mbunge fedha ninazoingiza
kupitia muziki huwa zinatumika kununua sare, na mahitaji mengine ya
shule kwa watoto yatima, na wale waishio kwenye mazingira magumu Jijini
Mbeya.”
Sugu
ni miongoni mwa wasanii wa zamani wa muziki wa Hiphop ambao baadaye
waliamua kujiingiza kwenye siasa na kushinda ubunge kupitia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
mPEKUZI.
Comments