Shirika la Kufuatilia Turathi za Kale nchini India limetangaza kwamba mahakama kuu ya nchi hiyo, imewataka Waislamu wa Taj Mahal kutoswali swala ya jamaa isipokuwa tu siku za Ijumaa.
Kutokana na uamuzi huo, mkuu wa kamati ya uongozi wa msikiti mkuu wa Taj Mahal, sambamba na kupinga hukumu hiyo ya mahakama kuu yai India amesema kuwa, hakuna sababu yoyote inayohalalisha kusimamishwa swala ya jamaa katika eneo hilo kwa kuwa swala hiyo imekuwepo kwa kipindi kirefu katika mji huo wa kihistoria.
Hii ni katika hali ambayo shakhsia kadhaa wa India wamekosoa misimamo ya serikali ya New Delhi kutokana na kuwa na mtazamo hasi dhidi ya dini ya Kiislamu.
Wakati huo huo Waislamu nchini humo pamoja na imam wa swala ya jamaa mjini Taj Mahal, Sayyid Swadiq Ali, ambaye familia yake imekuwa ikisimamia swala ya jamaa mjini hapo kwa miongo kadhaa, pia wamepinga uamuzi huo wa mahakama ya India.
Inafaa kuashiria kuwa, Taj Mahal ni moja ya mifano ya kuvutia zaidi ya mchanganyiko wa usanifu majengo wa Kihindi na Kiislamu, jengo ambalo liliasisiwa mwaka 1631 Miladia na kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016 za serikali ya India, watu milioni 6.5 hulitembelea jengo hilo kila mwaka.
Comments