Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema marekebisho ya
Sheria ya Takwimu ya mwaka 2018 hayana lengo la kuzuia watu, taasisi au
vyuo kufanya utafiti.
Dk.Kijaji ametoa kauli hiyo jana jijini Dodoma katika Maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika.
Alisema
kuwa madhumuni makubwa ya marekebisho na uridhiaji wa Mkataba wa
Takwimu wa Afrika ni kuhakikisha kuwa zinazalishwa takwimu ambazo
zinazingatia viwango.
“Niwatoe
wasiwasi wananchi na wadau mbalimbali kwamba marekebisho haya yana
lengo jema na hayana lengo la kuzuia kufanya tafiti,”alisema.
Kadhalika,
alisema Wizara hiyo ipo katika hatua ya kuandaa kanuni za utekelezaji
wa marekebisho hayo na wadau watashirikishwa ili kuwe na uelewa wa
pamoja wakati wa utekelezaji wa sheria hiyo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mpekuzi.
Comments