Naibu wa Oparesheni za jeshi la Iran: Meli za Iran zitaendelea kuwepo katika maji huru.

Naibu wa Oparesheni za jeshi la Iran: Meli za Iran zitaendelea kuwepo katika maji huruNaibu Kamanda wa oparesheni za jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Meli za vikosi vya majini zitaendelea kuwepo katika maji huru kwa lengo la kudhamini maslahi ya Iran. 

Admeli Sayyid Mahmoud Mousavi Jumapili hii aliashiria namna vikosi vya majini vya Iran vilivyo na nguvu na kueleza kuwa Iran ni nchi inayopakana na bahari na kwa msingi huo inapasa kuwepo siku zote katika maji ya kimataifa. 

Admeli Mousavi amesema kuwa suala la kuwatuma wanajeshi wa majini katika bahari ya Atlantic lipo pia katika ajenda ya kazi na kuongeza kuwa: Kuwepo wanajeshi wa majini wa Iran katika bahari ya Atlantic kutafanyika kulingana na wakati na pale itakapohitajika kwa mujibu wa mahitaji na agizo la uongozi wa juu. 
Kuhusu vikwazo vya kidhulma na vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran, Naibu Kamanda wa oparesheni za jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwekewa vikwazo kama hivyo vya kidhulma tangu mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu lakini hatua kwa hatua nchi hii imeweza kupiga hatua kubwa za maendeleo.  

parstoday.

Comments