Mufti Zuberi atoa msimamo wa ushonga Tanzania.

Mufti wa Tanzania Bara, Sheikh Abubakar Zuberi, ametumia Baraza la maulid kuwataka masheikh wa mikoa nchini, kukemea vitendo vya ushoga ambavyo vinaharibu sifa ya uislamu.

Alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi katika kumbukizi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) inayofanyika kitaifa Wilaya ya Korogwe jijini Tanga.

Alisema jambo la ushoga nchini halikubaliki na linapaswa kupingwa kwa nguvu zote.

“Jambo la ushoga halikubaliki, haiwezekani nchi tukufu kama Tanzania kuwa na vitendo hivi, masheikh lisemeeni jambo hili ili tunusuru umma na Taifa kwa ujumla,” alisema.

Baraza hilo limeongozwa na Waziri wa Nchi, Tamisemi, Selemani Jafo, kwa niaba ya Rais John Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali.

Akizungumza katika baraza hilo, Jafo aliwaomba waislamu kuendelea kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuwaletea maendeleo watanzania.

zanzibarleo.

Comments