Raia wa Tanzania amekamatwa akiwa ameficha mihadarati kwenye njia yake ya kwenda haja kubwa (rektamu).
Walikuwa safarini kuelekea China na India walipokamatwa Alhamisi usiku katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Mtanzania
huyo ambaye ametambuliwa na idara ya uchunguzi wa jinai nchini Kenya
kama Msafiri Musa alitoa tembe 47 za dawa za kulevya mara ya kwanza.
Aliwekwa
chini ya uangalizi ambapo baadaye alitoa tembe nyingine 69. Polisi
hawajasema raia wa mataifa hayo mengine ni kina nani.
"Wachunguzi
wa jinai wamewasilisha maombi katika mahakama ya JKIA kumzuilia zaidi
ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi. Washukiwa bado wanaendelea
kuangaliwa kwa makini," idara ya uchunguzi wa jinai Kenya imesema
kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Credit: BB na Mpekuzi.
Comments