Askari
watatu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia wakati
wakiwa kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa (UN) wameagwa leo
Lugalo huku vilio na hali ya kuzimia ni baadhi ya mambo yaliyotawala
wakati waombolezaji walipoishuhudia miili ya wapendwa wao.
Askari
hao waliuawa wakiwa kwenye majukumu ya ulinzi wa amani katika Jamhuri
ya ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni Praiveti Mussa Shija Machibya na
Koplo Mohammed Mussa wakati Koplo Erick Masauri John alipoteza maisha
akiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Askari wote waliuawa baada ya kushambuliwa na vikosi vya waasi vinavyoendesha mapigano katika maeneo ya msituni.
Shughuli
za kuagwa askari hao zimefanyika katika viwanja vya hospitali ya Lugalo
na kuhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk
Hussen Mwinyi, vikosi vya ulinzi na usalama na ndugu na jamaa.
Waziri Mwinyi ndiye aliyeanza kutoa heshima za mwisho na baadaye kufuatiwa na maofisa wa jeshi kabla ya ndugu kumalizia.
Wakati
wakitoa heshima zao baadhi ya ndugu walionekana kuzidiwa kiasi cha
wengine kuzimia hali iliyofanya watoa huduma ya kwanza kuwasaidia.
Miili ya askari hao iliyowasili jana imesafirishwa katika mikoa ya Mara, Mwanza na Zanzibar ambako itazikwa.
Mpekuzi.
Comments