Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajiwa kutoa uamuzi utakaotoa mustakabali
wa dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime
Mjini, Esther Matiko wanaokabiliwa na kesi ya jinai mahakamani hapo leo.
Uamuzi
huo unatokana na maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka Novemba 12,
uliodai washtakiwa hao wamekiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya
nchi bila kibali cha mahakama na kushindwa kuripoti katika kituo cha
Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala.
Upande
wa mashtaka ulifikia hatua hiyo baada ya Mbowe kushindwa kufika
mahakamani, Novemba Mosi na 8 na Matiko kushindwa kufika Novemba 8, kwa
ajili ya usikilizwaji wa awali wa kesi inayowakabili.
Katika
uamuzi huo utakaotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri
anayesikiliza kesi hiyo ndiyo utakaotoa hatima ya wabunge hao wa Hai na
Tarime Mjini iwapo wataendelea kubaki uraiani au watatupwa rumande.
Kama
Mahakama itaridhika na utetezi wao, itatupilia mbali hoja na mambo ya
upande wa mashtaka na hivyo wataendelea kuwa nje kwa dhamana wakati kesi
yao ikiendelea kusikilizwa na kusubiri uamuzi.
Lakini
kama mahakama hiyo itakubaliana na maombi na hoja za upande wa mashtaka
na kutupilia mbali utetezi wao, inaweza ikawafutia dhamana na kuamuru
watupwe mahabusu.
Kama
mahakama katika uamuzi wake itawafutia dhamana, huo hautakuwa mwisho
wao wa kusaka kurejesha haki hiyo ya kuwa huru kwa dhamana.
Washtakiwa
wanaweza kuomba tena dhamana kupitia kwa hakimu huyohuyo au kukata
rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu.
Au
wanaweza kuomba tena dhamana lakini hiyo inaweza kuwa na ugumu
kufanikiwa kwa sababu Mahakama ina uhuru wa kuwapatia tena dhamana au
kuwanyima, kwa kutegemeana na hoja watakazozitoa.
Mpekuzi.
Comments