Naibu waziri, Dk. Makame Ali Ussi, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, ofisini kwake Maruhubi.
Alisema mradi huo umelenga kuchimba visima 49 na ujenzi wa mabwawa ya
maji katika maeneo ya mabonde ya mpunga Unguja na Pemba ambapo heka
1,524 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
Alisema mabonde mengine kwa maumbile yake lazima yachimbiwe visima
ikiwemo Cheju ambapo visima 39 vinatarajiwa kuchimbwa, Kibokwa 10 na
Kilombero sita.
Mengine ni Chaani, Kinyasini kwa Unguja na Mlimele na Makwararani Pemba ambapo kila bonde kutachimbwa bwawa moja.
Alisema wanahitaji kuzalisha mchele wa kutosha hivyo anaamini mradi huo utakuwa na mafanikio.
Alisema mradi huo ni mkombozi katika uzalishaji wa mpunga hivyo inawezekana Zanzibar ikajitosheleza kwa chakula siku za usoni.
Alisema uchimbaji wa visima unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
Zanzibarleo.
Comments