Mku
wa wilaya ya Micheweni Mh. Salam Mbarouk Khatib amesema michezo nimuhimu katika
kujenga afya za binadamu hivyo nivyema kila mmoja kuipa umuhimu wakipee.
Ameyasema
hayo wakati akikabidhi Kombe la ujirani mwema kwa timu ya Combain iliyo ibuka
kidedea dhiri ya Beach Boys katika michuano hiyo iliofanyika kiwanja cha maji
maji Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema
kutokana na umuhimu wa mchezo huo ulioipa hadhi kubwa Wilaya yake ameamua
kutangaza michuano ya SALAMA CUPA ambayo itatoa motisha kwa timu za wilaya
hiyo.
Alifafanua
kuwa nifaraja kuona timu za wilaya ya micheweni kuipa umuhimu wa kuanzisha ligi
zao wenyewe nakuahidi kama Kiongozi wa wilaya hawezi kubaki nyuma nakutangaza
kutoa nguvu zaidi kupitia ligi itakayo anzishwa hivi karibuni ya salam cup.
“Nimejifunza
mengi leo kutoka ndani ya mchezo huu na nikupongezeni timu zote zilizo shiriki
Kombe la Ujirani Mwema pamoja na viongozi wote bila kujali mukaamua
kulifanikisha hili” Alisema Salama.
“leo
naomba nitangazieni ligi ambayo mimi mwenyewe nitaianzisha naipa jina la SALAMA
CUP hii itazidisha mapenzi hasa kwa wilaya yetu”.
Katika
mchuano kati ya Comban na Beach Boys ulimalizika kwa penalt zilizo ipa ushindi
mkali timu ya Comban wa mabao 3 kwa 2 nakulazimisha kuwa washindi wa Kombe la
Ujirani Mwema lilioanzishwa na Viongozi wa Jimbo la Tumbe Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba.
![]() |
Mh. salama akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Beach Boys |
![]() |
Mh. salama Akimpatia maelekezo golkipa wa timu ya Beach Boys Juu ya kujenga heshima katika mchezo. |
![]() |
Mkuu wa wilaya ya micheweni Mh. Salama Mbarouk Khatib akikagua timu kabla ya mchezo kuanza. |
![]() |
Mkuu wa wilaya ya micheweni salama Mbarouk Khati akiwa na katibu tawala wa wilaya ndogo ja kojani kushoto. |
![]() |
Mkuu wa wilya ya Micheweni akisalimiana na wachezaji wa timu ya Combain. |

Comments