Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Yazifungia benki tano kuuza na kununua dola.....Barclays, Exim Watoa Ufafanuzi.
Benki
Kuu ya Tanzania (BoT) imezifungia kwa mwezi mmoja benki za kibiashara
tano kutojihusisha na ubadilishaji wa fedha za kigeni kutokana na sababu
ambazo bado hazijawekwa wazi.
Hatua
hiyo ya BoT inatazamwa kama mwendelezo wa chombo hicho kikuu cha
usimamizi wa fedha kudhibiti biashara ya utakatishaji na ubadilishaji wa
fedha kiholela.
Takriban
wiki mbili zilizopita BoT iliyafungia maduka kadhaa jijini Arusha kwa
madai kuwa yanaendesha shughuli zake kinyume na sheria zinazosimamia
biashara hiyo, baada ya hapo ilitangaza kuwa huduma za ubadilishaji
fedha zitapatikana katika hoteli za kitalii, benki na ofisi zao.
Kwa
mujibu wa taarifa ya BoT, benki zilizofungiwa kufanya biashara ya
ubadilishaji fedha kuanzia Novemba 23 ni Barclay, Exim, UBA, ABC na
Azania.
“Hatua
hii imetokana na kuvunjwa kwa taratibu na kanuni, waliofungiwa walikuwa
aidha wanafanya biashara kinyume na viwango vinavyowekwa au walikuwa
hawawasilishi taarifa za miamala waliyokuwa wanafanya,” alisema
Alexander Mwinamila ambaye ni mkurugenzi wa masoko ya fedha wa BOT.
Aliongeza
kuwa hatua iliyochukuliwa inalenga kusimamia kanuni na taratibu za soko
la ubadilishaji fedha za kigeni kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
Barclays Tanzania na Exim Wametoa ufafanuzi hapo chini
Mpekuzi.
Comments