Balozi Seif amtembelea Nyanga.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema serikali bado inaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ili kuhakikisha ustawi wao unaimarika.

Alisema hayo wakati akimjuilia hali Waziri wa zamani, Suleiman Othman Nyanga, nyumbani kwake Mpendae mjini Unguja.

Alisema zipo taratibu zilizowekwa na serikali kupitia wizara ya afya za kumpatia uhamisho mgonjwa awe kiongozi au mwananchi wa kawaida wa kupelekwa matibabuni Tanzania Bara au nje ya nchi iwapo hali ya afya yake inakuwa mbaya asa kutokana na ukosefu wa vipimo au utaalamu.

Alimuhakikishia waziri huyo wa zamani wa Zanzibar kwamba serikali itaendelea kumpa msaada wakati wowote pale atakapohitaji kulingana na afya yake licha ya kupangiwa kurejea tena matibabuni nje ya nchini mwanzoni mwa mwaka ujao.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao pia walizungumzia hali ya soka visiwani Zanzibar ambapo Balozi Seif akimkumbusha Nyanga enzi zake wakati alipokuwa mchezaji wa kutegemewa wa timu ya soka ya Miembeni wakati yeye akiwa kipa wa timu ya Ujamaa.

Zanzibarleo.

Comments