Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyemba amesema akifika Tanzania atamueleza Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa kilichotokea kwenye mchezo dhidi ya Lesotho kuwa ni bahati mbaya na kumuahidi kuwa kwenye mechi dhidi ya Uganda Taifa Stars itaibuka na ushindi.
Dkt Mwakyembe ametoa kauli hiyo baada ya mchezo dhidi ya timu ya Lesotho na Taifa Stars jana Novemba 18, ambapo Taifa Stars ilifungwa bao 1-0.
Akizungumza na waandishi wa habari Nchini Lesotho Waziri Mwakyembe amesema; “ Raisa alisema turudi na ushindi, nitamwambia tumefungwa moja na tunasubiri mechi ya Uganda ambayo lazima tushinde, huu ndiyo moyo wa kimchezo, ukijikunyata utakuwa unadundwa ngumi kila wakati.
“Milioni 50 tulizopewa zimetusaidia kufungwa bao moja tu pengine tungefungwa hata sita ila tumefungwa sawa ndiyo mchezo tunaendelea kutafuta ushindi, tumejitahidi sana ila kwa sasa sio kichwa cha mwendawazimu tena,” ameongeza Mwakyembe.
Jana Rais Magufuli alieleza kuufatilia mchezo baina ya timu ya Taifa dhidi ya Lesotho ambapo katika mtandao wa Twitter aliandika; "vijana wangu Taifa Stars, muda mfupi ujao nitakuwa nikitazama mchezo kati yenu na timu ya taifa ya Lesotho, mimi na Watanzania wenzangu tunawatakia mchezo mwema, mrudi na ushindi,".
Comments