Hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa mradi huo, ilifanyika jana kati ya
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na kampuni ya kichina ya
CRJE.
Akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa
ZSSF, Sabra Issa Machano, alisema mradi huo utakamilisha mwishoni mwa
mwaka 2020.
Alisema mradi huo utakaogharimu shilingi bilioni 27.9, utahusisha
sehemu tatu ikiwemo maduka 37, nyumba za makazi 20, pamoja na maegesho
ya gari.
Alisema ujenzi wa maegesho ya gari utapunguza changamoto iliyopo
ambayo inasababisha watu kuegesha gari bila kuzingatia utaratibu.
Alisema anaamini mradi huo utakuwa na tija kwa mfuko na kuongeza mapato ya serikali.
Alisema uteuzi wa kampuni hiyo unatokana na kuwasilisha zabuni yenye
kiwango cha chini cha fedha ikilinganishwa na kampuni nyengine
zilizoomba kujenga mradi huo, ambapo kampuni 28 zilijitokeza.
Alisema anaamini mradi huo utakuwa na viwango na utakamilika ndani ya muda uliokubaliwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya ZSSF, Suleiman Rashid Mohammed,
aliitaka kampuni ya CRJE kujenga mradi huo kwa kiwango kinachokubalika.
Zanzibarleo.
Comments