‘Zaidi ya watalii 2.33 walitembelea Z’bar’.

ZAIDI ya watalii milioni 2.35 walitembelea Zanzibar kuanzia mwaka 2010 hadi Julai mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Sabahi Saleh Ali, wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Amani.
Alisema watalii hao waliingia nchini kwa kutumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume na bandari ya Malindi.
Aidha alisema, kuongezeka kwa mashirikia ya ndege yanayotoa huduma Zanzibar, yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini
Alisema kwa mwaka 2018, Zanzibar inatarajia kupokea watalii 264,262, ambapo fedha watakazotumia zitasaidia serikali katika kuwapekea maendeleo wananchi wake.
Aidha alisema, mpango wa baadhi ya hoteli kuandaa tamasha la vyakula na matembezi ya gari za zamani, kumesaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini.
Mwenyekiti huyo, alisema tamashala la kimataifa la utalii linalotarajiwa kufanyia baadae mwezi huu, litakuwa sehemu ya kivutio cha utalii, ambapoaa watalii watapata fursa ya kujionea vivutio mbali mbali vilivyopo nchini.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, walisema bado mikakati zaidi inahitaji kuchukuliwa ili kuifanya Zanzibar kituo cha watalii wa daraja la kwanza duniani.

Zanzibarleo.

Comments