Taarifa ya WHO imeeleza kwamba, maradhi ya Ebola yanatarajiwa kuenea na kusambaa katika nchi jirani za Uganda na Rwanda katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo.
Aidha sehemu nyingine ya taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa jana Alkhamisi imeeleza kuwa, nchi jirani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimejiandaa vizuri kukabiiliana na maradhi ya Ebola lakini hazijaafiki na kuidhinisha chanjo ya maradhi hayo.
Wakati huo huo, Shirika la Afyya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, idadi ya watu waliopoteza maisha yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na ugonjwa wa Ebola imeongezeka na kufikia 122.
Watoto watatu ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha hivi karibuni, kwa mujibu wa maafisa wa wizara ya afya. Inaripotiwa kuwa, watu wengine sita waliopoteza maisha ni wakaazi wa mji wa Beni ulioko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Uganda.
Mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola ulianza tarehe 8 Mei mwaka huu katika mji wa Bikoro kwenye mkoa wa Équateur huko kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia yya Congo na baadaye maambukizi ya ugonjwa huo yalihamia katika mji wa Mbandaka ambao ndio makao makuu ya mkoa huo.
Itakumbwa kuwa, kuanzia mwishoni mwa mwaka 2013 hadi 2016 ugonjwa huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 11 na 300 katika baadhi ya nchi za magharibi mwa Afrika.
Comments