Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba Aipinga Ripoti ya Polisi Kuhusu Ajali Iliyoua Wafanyakazi Watano wa Wizara Hiyo.
Waziri
wa Kilimo Dk Charles Tizeba amepinga taarifa ya Polisi Mkoa wa Singida
kuhusu ajali ya gari ya wizara hiyo iliyosababisha vifo vya wafanyakazi
watano wa wizara.
Ajali hiyo ilitokea Jumapili Oktoba 21 mkoani Singida baada ya gari lao aina ya Mitsubishi Pajero kugongana uso kwa uso na lori.
Muda
mfupi baada ya kutokea ajali hiyo zilisambaa picha katika mitandao ya
kijamii zikionyesha gari hiyo kuwa katika spidi 89 katika eneo lenye
kibao kinachoonyesha spidi inayotakiwa ni 50.
Akitoa
salamu za rambirambi katika ibada ya mazishi ya watumishi hao leo
Oktoba 23, 2018, Dk Tizeba amesema jana alitumia muda mwingi kuzungumza
na wananchi na dereva wa roli lililosababisha ajari hiyo.
"Nawaomba
polisi wa Singida warudie taarifa zao, wamehukumu na mitandao
mbalimbali nayo imehukumu. Hili si kweli hata kidogo. Napinga taarifa
zile zimejaa upotoshaji na hukumu isiyo ya kweli," amesema Tizeba.
Waziri
Tizeba amesema mita chache kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo kuna tuta
kubwa ambalo gari haliwezi kupita likiwa katika mwendo mkali.
Hata
hivyo, amekiri dereva wa gari hilo alikuwa akiyapita magari mengine na
kwamba lori lililogongana na gari hilo la wizara lilikuwa limeegeshwa
pembeni lakini liliingia ghafla barabarani.
Watumishi
hao ni Stella Joram Ossano (39), Esta Tadayo Mutatembwa (36), Abdallah
Selemani Mushumbusi (53), Charles Josephat Somi na Erasto Mhina (43).
Mpekuzi.
Comments