Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknologia Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba
wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma kwa kipindi cha miaka
saba kama ilivyokuwa awali.
Profesa
Ndalichako aliyasema hayo mjini Pangani wakati wa Kongamano la Elimu
wilayani Pangani lililoenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa
mabweni ya wanafunzoi shule ya sekondari Mwera mbapo alisema suala la
muda wa elimu msingi lipo kwa mujibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1982.
Alisema sheria hiyo imeweka bayana kwamba muda wa elimu ya msingi ni miaka saba na bado sheria hiyo haijafanyiwa marekebisho hivyo wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma miaka saba.
Akitolea
ufafanuzi suala hilo alisema ikifika mahali kama kutakuwa na ulazima wa
kubadilisha miaka ya kwenda shule kitakachotanguliwa ni kufanya
marekebisho ya sheria kwa sababu jambo linalokuwa ndani ya sheria huwezi
kulifanyia mabadiliko bila kuanza kufanya marekebishi ya sheria husika.
“Niwatoe
hofu watanzania kwamba suala la kisheria huwezi kubadilika kwa tamko
wala waraka wa kamishna wa elimu au kubadilika kwa maelekezo mengine
yoyote bali linaweza kubadilika pale sheria ya elimu 1982 kwenye
kipengine kinachoeleza muda wa elimu ya msingi miaka 7 kitakapofanyiwa
marekebisho”Alisema Waziri Profesa Ndalichako
Alisema
baada ya kufanyiwa marekebisho ndio inaweza kubadilika na haitakuwa
kinyumenyume na itaweka bayana kwa sababu badiliko kama hilo ni kubwa la
sera na kisheria hivyo watu watafahamu mapema.
“Kumekuwa
na mchanganyika kwa sababu sera ya elimu ya mwaka 2014 imeonyesha
serikali itakuja kuweka utaratibu lakini haikusema itaweka lini kwamba
elimu ya msingi iwe lazima mpaka sekondari”Alisema.
Alisema
bado hatujawa tayari kuwa elimu ya msingi na sekondari kwa wanafunzi
wote hivyo tunaendelea kuboresha elimu ya msingi na sekondari
kuhakikisha mazingira mazuri ya kufundisha na walimu wa kutosha.
Alisema
watakapoona wamefika mahali na kuona haja ya kufanya hayo watu wamekuwa
wakiulizia serikali itawashirikisha wadau wote kwamba tunakwendaje huku
akieleza mkakati ni serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia na
kufundishia.
Mpekuzi.
Comments