Na Ahmed Mahmoud, Arusha
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa
kufunga maadhimisho ya tamasha la mwezi wa Urithi wa Utamaduni mkoani
hapa
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini hapa jana na kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha
Theresia Mahongo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Karatu, alisema
maadhimisho hayo yatafanyika wilayani Karatu kuanzia Oktoba nane mwaka
huu.
Alisema
maadhimisho hayo ambayo yalizinduliwa Jijini Dodoma Septemba 15 mwaka
huu na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan yaliendelea kufanyika maeneo
mbalimbali nchini ikwemo Zanzibar,Mwanza na Dar es Salaam.
Alisema
kabla ya kilele hicho maadhimsho hayo yatafanyika kwa siku tano
kuanzia Oktaba nane hadi 12 wilayani Karatu kwenye viwanja vya
mazingira ambapo yatakwenda sambamba na maonyesho mbalimbali ya
kiutamaduni.
“Maadhimisho
haya yenye jina la “Urithi Festival Celebrate our Heritage kimkoa
yataanza kuadhimishwa wilayani Karatu kuanzia Oktoba 8 na kilele
caheke kitakuwa Oktoba 13 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
uliopo Jijini Arusha”.
Aliongeza”Maonyesho
hayo yatashirikisha ngoma za makabila 10 ya mkoa huu,maigizo,kutembelea
vituo mbalimbali vya utalii pamona na michezo mbalimbali ya asili”
Licha
ya maonyesho hayo pia wananchi wa mkoa wa Arusha watapata fursa ya
kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kitamaduni ikwemo makumbusho
mbalimbali na bonde la Ngorongoro kwa gharama ndogo.
Mpekuzi.
Comments