
Alisema kuwa shughuli za utoaji wa matibabu kwa kutumia
tiba asili ,matangazo ama kisomo bila ya kuwa na kibali ama leseni ya
kuruhusiwa kufanya kazi hiyo nikinyume na utaratibu kwa baraza la tiba
asili ba tiba mbdala hapa Zanzibar.
Kauli hiyo ameitoa huko kijiji cha Raha Shehia ya Ukunjwi
Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipofika kumkamata
Ibrahim Suleiman alokuwa akiendesha shughuli hizo za tiba asili kwa njia
ya kisomo na kuwapatia dawa wagonjwa hao bila jambo ambalo ni makosa
kwake kwani amekiuka sheria ya baraza la tiba asili na tiba mbadala
kwamba kila mtu anatakiwa kuwa na leseni ya kazi hiyo.
"Ndugu yetu Ibrahim hii ni mara ya pili kumkamata
akiendesha shuguli za utoaji wa matibabu asilia kwa kisomo cha cha
kurani katika mkusanyiko wa watu kinyume na sheria zetu na leo
nimechukua nafasi hii ya kumkata na kumfikisha kituoni ili kumchukulia
hatua za kisheria kwani amekua akikaidi magizo yetu" alisema .
Alifahamisha kitengo kinachoruhusu kufanya kazi hizo za
tiba asili ni baraza la tiba asili na tiba mbadala pekee na sio sehemu
yenyengine yoyote wao ndio wanao husika na masuala hayo tu na kutoa
mamuzi.
Aidha alifahamisha kuwa sheria ya baraza la tiba asili na
tiba mbadala limeweka faini kwa mtu yoyote ambae ata kamatwa akifanya
kazi hiyo bila kibali kulingana biashara wenyewe na kazi ilivyo kwa
kuanzia kiwango cha laki tatu na kwenda juu.
"Faini zetu zinategemea na kazi wenyewe kama alivyo ifanya
ndg yetu Ibrahm faini yake yeye ni Shilingi laki tatu na nimemtaka
akailipie benki pesa hiyo ili kuondokana na usumbufu kwenye kazi
yake".alifahamisha.
Kwa upande wake mtoa huduma hiyo Ibrahim Suleiman ,alikiri
kufanya kazi hiyo bila ya kuwa na kibali kinacho mruhusu kufanya kazi
hizo na kumtaka Mkuu huyo wa baraza la tiba asili na tiba mbadala
kumpunguzia faini hiyo kwa vile amekubali kutenda kosa kinyume na
sheria za baraza hilo.
Nae Mzee Khamis Said Ali, aliyekuwa akipatiwa huduma hiyo
ya kisomo alisema alifika hapo kupatiwa dua kwani anasumbuliwa na
matatizo ndani ya mwili wake na kusema mtibabu huyo anawadanyia tiba
hiyo bila ya kuwatoza pesa kinyume na kauli za watu wanazosema kwamba
anawadai Eflu Thalathini baada ya kumaliza matibabu hayo.
Na mwandishi wetu.
Comments