Hayo yalielezwa na Meneja wa mradi wa kuijengea uwezo jamii kuhusu kujikinga na kudhibiti maradhi yasiyoambukiza, Haji Khamis Fundi, ofisini kwake Mpendae wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema njia za kujikinga na maradhi hayo ni pamoja na jamii kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara na kuepuka kutumia vyakula vyenye mafuta.
Alisema njia nyingine ni pamoja na kufanya mazoezi ya viungo na kutumia vyakula vya asili.
Akielezea kuhusu mradi huo, alisema lengo ni kujenga uwezo wa muungano wa jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi yasiyoambukiza ili iweze kushirikiana na jamii kujikinga na kudhibiti maradhi hayo.
Alisema kupitia mradhi huo wametoa huduma za upimaji wa maradhi mbali mbali ikiwemo sukari, macho na sindikizo la damu ambapo jumla ya watu 1,125 walifanyiwa vipimo.
Aidha kupitia mradi huo watoto 283 walipatiwa mafunzo ya lishe ikiwemo kupiga mswaki.
Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi yasiyoambukiza, (ZNCDA) Louis Majaliwa, alisema jumuiya hiyo imeundwa na jumuiya za watu wanaoishi na maradhi hayo ikiwemo kisukari, saratani na moyo.
Zanzibarleo.
Comments