
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa kutoa elimu juu ya
utafiti wa mafuta na gesi huko Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini
Pemba Afisa mdhamini wizara ya ardhi, nyumba maji
na nishati Juma Bakar Alawi amesema nivyema kwa wananchi kuwa na tahadhani
kwani mionzi inayo toka katika zoezi hilo ina madhara kwa afya za binadamu.
Amefahamisha
kuwa nivyema kwa wananchi kufuata miongozo itakayo tolewa wakati zoezi hilo litakapoa
anza katika maeneo yanayo lengwa kuendeshwa tafiti hizo.
Amesema
kuwa lengo la serekali si kumuonea mwananchi bali nikujaribu kutumia hekma
ilikuona wanendelea kuishi katika hali ya usalama na amani bila athari zozote.
Sambamba
nahayo amewataka wananchi kuwa wasikivu na kuwa walimu kwa wengine ilikuona
mafanikio yanafikiwa bila kuwepo malalamiko yasio yalazima.
"najua wananchi sio wakaidi fuateni sheria kwani miozi hiyo inananadhara kwa wanadamu basi tuambizane ili kuepuka madhara hayo."
Jumla ya
shehia 30 zimepatiwa elimu uwelewa kabla ya zoezi hilo kuanza katika ukanda wa
bahari kisiwani Pemba.
Comments