Wakiongea na Sauti ya Amerika viongozi
wa elimu katika mkoa huo wamesema wanafunzi laki moja na nusu wa shule
za msingi katika mkoa huo, walikuwa wanapatiwa msaada wa chakula kutoka
shirika hilo, kwa kupata mlo skuli ili wasiache skuli baada ya
kudhihirka kwamba familia zao zinakabiliwa na umaskini.
Hiyo ni moja ya athari ya hatua ya
serikali ya Burundi kusitisha shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali
(NGOs ) 130 tangu tarehe mosi Oktoba, kwa madai kuwa mashirika hayo ya
hisani hayaheshimu sheria mpya inayoongoza shughuli za mashirika ya
kimataifa ya kigeni.
Serikali ilitowa masharti kadha kwa
mashirika hayo na kuyapa muda wa miezi mitatu ili yawe yamekwisha
tekeleza masharti hayo ili yaweze kuendele kufanya kazi.
Baadhi ya masharti hayo, ni pamoja na
mashirika hayo ya kigeni kuweka pesa zao zote za matumzi za kigeni
kwenye benki kuu ya taifa na kuhakikisha usawa kati ya makabila muhimu
ya Burundi wakati wa kuajiri wafanyakazi.
Wakati hayo yakijiri, wawakilishi wa
nchi zinazofadhili NGOs hizo ambazo ni Marekani, Canada, Japan, USwiss,
Umoja wa Ulaya na Shirika la Umoja wa Mataifa linalo simamia maendeleo
(UNDP), wametowa tamko kwa vyombo vya habari wakiomba kuwepo mazungumzo
zaidi na Serikali ya Burundi, ili kupata mwanga na muwafaka kuhusu
masharti yaliotolewa.
Katika tamko hilo, wawakilishi wa nchi
hizo wamesema, “ tunaelewa matakwa ya serikali ya Burundi, lakini na
sisi tunaomba serikali kuelewa maadili na utaratibu wa nchi
zinazofadhili mashirika ya kimataifa ya hisani.”
Comments